2 years ago

Assalaamu aleykum.

As.alaykum, vipi ndugu zangu mupo? Munaendeleaje na masomo? Nawatakieni matayarisho mema ya ramadhani na mitihani.

2 years ago

Attension.

Assalaamu aleykum yaa ikhwaaniy, Kwamujibu wa mshika fedha takriban 60% ya members hawajatoa mchango wa mwezi march. So, nachukua fursa hii kuwakumbusha wale wote ambao walijisahau kutoa mchango huo.

2 years ago

Mchango.

Kumbuka kulipa mchango wa mwezi kwa wakati ndio kufanikiwa kwa jumuia.

2 years ago

Shule 10 bora zilizofanya vizuri mtihani wa kidato cha nne 2014.

Zifahamu Shule 10 Bora za mwanzo na 10 Zilizofanya Vibaya Mtihani wa “Form Four 2014″

Jumla ya Watahiniwa 196,805 sawa na 68.33% ya watahiniwa wote waliofanya mtihani kidato cha IV mwaka 2014 wamefaulu ikiwa niongezeko la 10.08% kulinganisha na mwaka 2013 ambapo wanafunzi 235227 sawa na 58.25 walifualu.

Katika matokeo hayo zipo shule zilizofanya vizuri. Shule bora 10 za mwanzo na  zile 10 za mwisho ambazo hazijafanya vizuri katika mtihani huo wa kidato cha nne Kitaifa;

Akizitaja shule kumi bora kwa ufaulu, Dkt Msonde amesema shule hizo ni;

 1. Kaizirege mkoa wa Kagera
 2. Mwanza Alliance mkoa wa Mwanza
 3. Marian Boys mkoa wa Pwani
 4. St. Francis Girls mkoa wa Mbeya
 5. Abbey mkoa wa Mtwara
 6. Feza Girls mkoa wa Dar es salaam
 7. Canossa Mkoa wa Dar es Salaam
 8. Bethel sabs Girls mkoa wa Iringa
 9. Marian Girls mkoa wa Pwani
 10. Feza Boys mkoa wa Dar es laam.

Shule 10 za mwisho ni;

 1. Manolo mkoa wa Tanga
 2. Chokocho mkoa wa Pemba
 3. Kwalugulu mkoa wa Tanga
 4. Relini mkoa wa Dar es salaam
 5. Mashindei mkoa wa Tanga
 6. Njelekela Islamic Seminary mkoa wa Kigoma
 7. Vudee mkoa wa Kilimanjaro
 8. Mnazi mkoa wa Tanga
 9. Ruhembe mkoa wa Morogoro
 10. Magoma mkoa wa Tanga.

 

2 years ago

Attention to PMO members.

All members of Pemba Mobile Educational Organization are required to visit this site for information about organization this site created by Amir to provide information to members about organization.

2 years ago

Performance of form four results 2014 of four schools in Mkoani - Pemba.

REPORT OF PERFOMANCE FOR THE YEAR 2014/2015.

Mizingani Secondary School is located at Pemba. Mizingani Secondary School is boys and girls school and it is doing well in Elimu ya dini ya kiislamu, Chemistry and Kiswahili than all subjects. Despite the effort in teaching, Mizingani Secondary School is still considered as red school S2414 O-level GPA 5.09

Regional rank 18/36

Less than 40 students.

Chokocho Secondary School is located at Pemba. Chokocho Secondary School is boys and girls school and it is doing well in Arabic language, Physics and Chemistry than all subjects. Despite the effort in teaching, Chokocho Secondary School is still considered as red school S4256 O-level GPA 5.56

Regional rank 33/34

More than 40 students.

Maendeleo Ngwachani Secondary School is located at Pemba. Maendeleo Ngwachani Secondary School is boys and girls school and it is doing well in Kiswahili, Elimu ya dini ya kiislamu and Biology than all subjects. Despite the effort in teaching, Maendeleo Ngwachani Secondary School is still considered as red school S1307 O-level GPA 4.79

Regional rank 7/36

Less than 40 students.

Wambaa Secondary School is located at Pemba. Wambaa Secondary School is boys and girls school and it is doing well in Arabic language, Kiswahili and Elimu ya dini ya kiislamu than all subjects. Despite the effort in teaching, Wambaa Secondary School is still considered as red school S1795 O-level GPA 4.89

Regional rank 10/36

Less than 40 students.

Mtambile Secondary School is located at Pemba. Mtambile Secondary School is boys and girls school and it is doing well in Arabic language, Elimu ya dini ya kiislamu and Kiswahili than all subjects. Despite the effort in teaching, Mtambile Secondary School is still considered as red school S1537 O-level GPA 4.63

Regional rank 4/34

More than 40 students.

 

2 years ago

TAARIFA KUTOKA WIZARA YA ELIMU ZANZIBAR.

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA AMALI ZANZIBAR

TAARIFA YA MATOKEO YA MTIHANI WA DARASA LA SABA NA KIDATO CHA PILI MWAKA – 2014

Mtihani wa Taifa wa darasa la saba ulifanyika tarehe 27/11/2014 na 29/11/2014 na ule wa kidato cha pili ulifanyika tarehe 01/12/2014 – 11/12/2014

Mwaka 2014 mtihani wa kidato cha pili ulishirikisha skuli binafsi na zile zenye michepuo.

MTIHANI WA DARASA LA SABA

•Wanafunzi walioandikishwa walikuwa 27,486 kati yao wanawake ni 14,297 na wanaume 13,189.

•Wanafunzi waliofanya mtihani 25,749 ni sawa na asilimia 93.7 ya wanafunzi walioandikishwa. Wanawake walikuwa 13,662 sawa na asilimia 95.6 na wanaume 12,087, sawa na asilimia 91.7.

•Wanafunzi 18,915 wamefaulu na kuchaguliwa kuingia kidato cha kwanza kwa masomo ya sekondari. Wanawake ni 10,618 na wanaume ni 8297 sawa na asilimia 73.5. Hii ni upungufu wa asilimia 4.3 ukilinganisha na mwaka uliopita 2013.

•Wanafunzi 105 wamefaulu na kuchaguliwa kuingia madarasa ya vipawa kati yao wanawake 53 na wanaume 52. Kutoka Unguja ni 84 wanawake 46 na wanaume 38 kutoka Pemba 21 wanawake 07 na wanaume 14. Hili ni ongezeko la asilimia 15.4 ukilinganisha na mwaka uliopita.

•Wanafunzi 1,558 wamefaulu na kuchaguliwa kuingia madarasa ya michepuo kati yao wanawake 790 wanaume 768, kutoka Unguja 1,105 wanawake 606 na wanaume 449 na kutoka Pemba ni 453 wanawake 184 na wanaume 269. Hili ni ongezeko la asilimia 15.7 ukilinganisha na mwaka uliopita.

SKULI BORA KWA JUMLA DARASA LA SABA

Kwa mwaka 2014 skuli zenye wastani mkubwa ukilinganisha na nyengine

1. Ali Khamis Camp. - Wilaya ya Chake chake.

2. Kibweni - Wilaya ya Magharibi.

3. Kinduni - Wilaya ya Kaskazini ‘B’

SKULI ZILIZOFANYA VIBAYA ZAIDI

1. Mwambe Shamiani - Wilaya ya Mkoani

2. Kigomani - Wilaya ya Kaskazini ‘A’

3. Birikau - Wilaya ya Chake Chake

MITIHANI WA KIDATO CHA PILI

•Wanafunzi 23264 waliandikishwa kufanya mtihani wa kidato cha pili, kati yao wanawake ni 12,431 na wanaume 10,833.

•Wanafunzi 21,944 waliofanya mtihani kati yao 11,825 wanawake na 10,119 wanaume. Hii ni sawa na asilimia 94.3 ya walioandikishwa.

•Wanafunzi 14,384 kati yao wanawake 8,011 na wanaume 6,373 wamefaulu. Na kuchaguliwa kujiunga na kidato cha tatu (Form III). Hii ni sawa na asilimia 65.6. Hili ni ongezeko la asilimia 6.2 ukilinganisha na mwaka uliopita.

Kwa jumla ufaulu wa wanawake ni asilimia 67.8 na ule wa wanaume ni 63.0. Hii inaonesha ufaulu wa wanawake ni mkubwa ukilinganisha na wanaume.

SKULI BORA KWA JUMLA KIDATO CHA PILI

Kwa mwaka 2014 skuli hizo ni hizi zifuatazo:

Skuli zenye wanafunzi 45 na zaidi

1.Zanzibar Commercial.

2.Mikindani Dole

3.Ben Bella

Skuli zenye wanafunzi chini ya 45

1.Feza

2.Kengeja Ufundi

3.Madungu

SKULI ZILIZOFANYA VIBAYA

Skuli zenye wanafunzi 45 na zaidi

1.Connecting Continent

2.Kiwani

3.Wambaa

Skuli zenye wanafunzi chini ya 45

1.Wete Islamic

2.Al-huda

3.Amini Islamic

KESI ZA UDANGANYIFU

Kwa mwaka 2014 kesi ya udanyanyifu ni 2 tu huu upunfufu mkubwa ukilinganisha na mwaka uliopita. Mwaka 2013 kasi za udanyanyifu zilikuwa 5.

WANAFUNZI BORA KITAIFA

DARASA LA SABA

1.YUSSUF HAMAD RAJAB - MITIULAYA

2.KHADIJA RAJAB SAID - M/KWEREKWE ‘B’

3.THABI KHAMIS KHAMIS - MTOPEPO ‘A’

KIDATO CHA PILI

1.SUMAIYA OMAR MUSSA - FEZA

2.SULEIMAN SALUM MASOUD - MADUNGU

3.KHALID RAJABU JUMA - MBARALI